Zechariah 6:2-7
2 aGari la kwanza lilivutwa na farasi wekundu, la pili lilivutwa na farasi weusi, 3 bla tatu lilivutwa na farasi weupe na gari la nne lilivutwa na farasi wa madoadoa ya kijivu, wote wenye nguvu. 4 cNikamuuliza malaika aliyekuwa akizungumza nami, “Hawa ni nani bwana wangu?”5 dMalaika akanijibu, “Hizi ni roho nne za mbinguni zisimamazo mbele ya uwepo wa Bwana wa dunia yote, zinatoka kwenda kufanya kazi yake. 6 eGari linalovutwa na farasi weusi linaelekea katika nchi ya kaskazini, la farasi weupe linaelekea magharibi na la farasi wa madoadoa ya kijivu linaelekea kusini.”
7 fWakati hao farasi wenye nguvu walipokuwa wakitoka, walikuwa wakijitahidi kwenda duniani kote. Akasema, “Nenda duniani kote!” Kwa hiyo wakaenda duniani kote.
Copyright information for
SwhNEN