Zechariah 4:1-5
Maono Ya Tano: Kinara Cha Taa Cha Dhahabu Na Mizeituni Miwili
1 aKisha malaika aliyezungumza nami akarudi na kuniamsha, kama mtu aamshwavyo kutoka usingizi wake. 2 bAkaniuliza, “Unaona nini?”Nikajibu, “Ninaona kinara cha taa cha dhahabu tupu, nacho kina bakuli juu yake na taa zake saba juu yake, tena iko mirija saba ya kuleta mafuta, kwenye taa zote zilizo juu yake. 3 cPia kuna mizeituni miwili karibu yake, mmoja upande wa kuume wa bakuli na mwingine upande wa kushoto.”
4Nikamuuliza malaika aliyezungumza nami, “Hivi ni vitu gani, bwana wangu?”
5 dAkanijibu, “Hujui kuwa hivi ni vitu gani?”
Nikajibu, “Hapana, bwana wangu.”
Copyright information for
SwhNEN