‏ Song of Solomon 4:12-15

12 aWewe ni bustani iliyofungwa, dada yangu,
bibi arusi wangu;
wewe ni chanzo cha maji kilichozungushiwa kabisa,
chemchemi yangu peke yangu.
13 bMimea yako ni bustani ya mikomamanga
yenye matunda mazuri sana,
yenye hina na nardo,
14 cnardo na zafarani,
mchai na mdalasini,
pamoja na kila aina ya mti wa uvumba,
manemane na udi,
na aina zote za vikolezo bora kuliko vyote.
15 dWewe ni chemchemi ya bustani,
kisima cha maji yatiririkayo,
yakitiririka kutoka Lebanoni.

Copyright information for SwhNEN
The selected Bible will not be clickable as it does not support the Vocabulary feature. The vocabulary is available by hovering over the verse number.