‏ Song of Solomon 4:11-14

11 aMidomo yako inadondosha utamu kama sega la asali,
bibi arusi wangu;
maziwa na asali viko chini ya ulimi wako.
Harufu nzuri ya mavazi yako ni kama ile ya Lebanoni.
12 bWewe ni bustani iliyofungwa, dada yangu,
bibi arusi wangu;
wewe ni chanzo cha maji kilichozungushiwa kabisa,
chemchemi yangu peke yangu.
13 cMimea yako ni bustani ya mikomamanga
yenye matunda mazuri sana,
yenye hina na nardo,
14 dnardo na zafarani,
mchai na mdalasini,
pamoja na kila aina ya mti wa uvumba,
manemane na udi,
na aina zote za vikolezo bora kuliko vyote.
Copyright information for SwhNEN