‏ Song of Solomon 2:8-17


Shairi La Pili

Mpendwa

8 aSikiliza! Mpenzi wangu!
Tazama! Huyu hapa anakuja,
akirukaruka juu milimani
akizunguka juu ya vilima.
9 bMpenzi wangu ni kama paa au ayala kijana.
Tazama! Anasimama nyuma ya ukuta wetu,
akitazama kupitia madirishani,
akichungulia kimiani.
10Mpenzi wangu alizungumza na kuniambia,
“Inuka, mpenzi wangu,
mrembo wangu, tufuatane.
11Tazama! Wakati wa masika umepita,
mvua imekwisha na ikapita.
12Maua yanatokea juu ya nchi;
majira ya kuimba yamewadia,
sauti za njiwa zinasikika
katika nchi yetu.
13 c dMtini unatunga matunda yake ya mwanzoni,
zabibu zinazochanua zaeneza harufu nzuri.
Inuka, njoo mpenzi wangu.
Mrembo wangu, tufuatane.”
Mpenzi

14 eHua wangu penye nyufa za majabali,
mafichoni pembezoni mwa mlima,
nionyeshe uso wako,
na niisikie sauti yako,
kwa maana sauti yako ni tamu,
na uso wako unapendeza.
15 fTukamatie mbweha,
mbweha wale wadogo
wanaoharibu mashamba ya mizabibu,
mashamba yetu ya mizabibu yaliyochanua.
Mpendwa

16 gMpenzi wangu ni wangu, nami ni wake,
yeye hujilisha katikati ya yungiyungi.
17 hMpaka jua linapochomoza,
na vivuli vikimbie,
rudi, mpenzi wangu,
na uwe kama paa,
au kama ayala kijana
juu ya vilima vya Betheri.
Copyright information for SwhNEN