‏ Romans 12:17-21

17 aMsimlipe mtu yeyote ovu kwa ovu. Jitahidini ili mtende yaliyo mema machoni pa watu wote. 18 bKama ikiwezekana, kwa upande wenu kaeni kwa amani na watu wote. 19 cWapendwa, msilipize kisasi, bali ipisheni ghadhabu ya Mungu, maana imeandikwa: “Ni juu yangu kulipiza kisasi, nitalipiza,” asema Bwana. 20 dBadala yake:

“Kama adui yako ana njaa, mlishe;
kama ana kiu, mpe kinywaji.
Kwa kufanya hivyo,
unaweka makaa ya moto yanayowaka kichwani pake.”
21Usishindwe na ubaya, bali uushinde ubaya kwa wema.

Copyright information for SwhNEN