‏ Romans 12:17-19

17 aMsimlipe mtu yeyote ovu kwa ovu. Jitahidini ili mtende yaliyo mema machoni pa watu wote. 18 bKama ikiwezekana, kwa upande wenu kaeni kwa amani na watu wote. 19 cWapendwa, msilipize kisasi, bali ipisheni ghadhabu ya Mungu, maana imeandikwa: “Ni juu yangu kulipiza kisasi, nitalipiza,” asema Bwana.
Copyright information for SwhNEN