‏ Revelation of John 18:3-9

3 aKwa maana mataifa yote yamekunywa
mvinyo wa ghadhabu ya uasherati wake.
Nao wafalme wa dunia wamefanya uzinzi nao,
nao wafanyabiashara wa dunia
wametajirika kutokana na wingi wa utajiri wake.”
4 bKisha nikasikia sauti nyingine kutoka mbinguni ikisema:

“Tokeni katikati yake, enyi watu wangu,
ili msije mkashiriki dhambi zake,
ili msije mkapatwa na pigo lake lolote;
5 ckwa kuwa dhambi zake zimelundikana hadi mbinguni,
naye Mungu ameukumbuka uhalifu wake.
6 dMtendee kama yeye alivyotenda;
umlipe mara mbili kwa ajili ya yale aliyotenda.
Katika kikombe chake mchanganyie
mara mbili ya kile alichochanganya.
7 eMpatie mateso na huzuni nyingi sawa na
utukufu na anasa alizojipatia.
Kwa kuwa moyoni mwake hujivuna, akisema,
‘Mimi ninatawala kama malkia;
mimi si mjane, wala sitaona huzuni kamwe.’
8 fKwa hiyo mapigo yatampata kwa siku moja:
mauti, maombolezo na njaa.
Naye atateketezwa kwa moto,
kwa maana Bwana Mungu amhukumuye ana nguvu.
9 g“Wafalme wa dunia waliozini naye na kushiriki anasa zake watakapoona moshi wa kuungua kwake, watamlilia na kumwombolezea.
Copyright information for SwhNEN
The selected Bible will not be clickable as it does not support the Vocabulary feature. The vocabulary is available by hovering over the verse number.