‏ Psalms 95:7-11

7 akwa maana yeye ndiye Mungu wetu,
na sisi ni watu wa malisho yake,
kondoo chini ya utunzaji wake.

Kama mkiisikia sauti yake leo,
8 bmsiifanye mioyo yenu migumu
kama mlivyofanya kule Meriba,
Meriba maana yake ni Kugombana.

kama mlivyofanya siku ile
kule Masa
Masa maana yake ni Kujaribiwa.
jangwani,
9 eambapo baba zenu walinijaribu na kunipima,
ingawa walikuwa wameyaona matendo yangu.
10 fKwa miaka arobaini nilikasirikia kizazi kile,
nikasema, “Hawa ni taifa ambalo mioyo yao imepotoka,
nao hawajazijua njia zangu.”
11 gHivyo nikatangaza kwa kiapo katika hasira yangu,
“Kamwe hawataingia rahani mwangu.”
Copyright information for SwhNEN