Psalms 89:24-28
24 aUpendo wangu mkamilifu utakuwa pamoja naye,kwa Jina langu pembe yake itatukuzwa.
25 bNitauweka mkono wake juu ya bahari,
mkono wake wa kuume juu ya mito.
26 cNaye ataniita kwa sauti, ‘Wewe ni Baba yangu,
Mungu wangu, Mwamba na Mwokozi wangu.’
27 dNitamteua pia awe mzaliwa wangu wa kwanza,
aliyetukuka kuliko wafalme wote wa dunia.
28 eNitadumisha upendo wangu kwake milele,
na agano langu naye litakuwa imara.
Copyright information for
SwhNEN