Psalms 83:1-12
Maombi Kwa Ajili Ya Kushindwa Kwa Adui Wa Israeli
Wimbo. Zaburi ya Asafu.
1 aEe Mungu, usinyamaze kimya,usinyamaze, Ee Mungu, usitulie.
2 bTazama watesi wako wanafanya fujo,
jinsi adui zako wanavyoinua vichwa vyao.
3 cKwa hila, wanafanya shauri dhidi ya watu wako,
wanafanya shauri baya dhidi ya wale unaowapenda.
4 dWanasema, “Njooni, tuwaangamize kama taifa,
ili jina la Israeli lisikumbukwe tena.”
5 eKwa nia moja wanapanga mashauri mabaya pamoja,
wanafanya muungano dhidi yako,
6 fmahema ya Edomu na Waishmaeli,
ya Wamoabu na Wahagari,
7 gGebali, ▼
▼Yaani Bubilo, mji wa zamani sana wa Ufoinike (kama kilomita 80 kaskazini mwa Beiruti).
Amoni na Amaleki,Ufilisti, pamoja na watu wa Tiro.
8 iHata Ashuru wameungana nao
kuwapa nguvu wazao wa Loti.
9 jUwatendee kama vile ulivyowatendea Midiani,
na kama vile ulivyowatendea Sisera na Yabini
hapo kijito cha Kishoni,
10 kambao waliangamia huko Endori
na wakawa kama takataka juu ya nchi.
11 lWafanye wakuu wao kama Orebu na Zeebu,
watawala wao kama Zeba na Salmuna,
12 mambao walisema, “Na tumiliki nchi
ya malisho ya Mungu.”
Copyright information for
SwhNEN