‏ Psalms 78:62-71

62 aAliachia watu wake wauawe kwa upanga,
akaukasirikia sana urithi wake.
63 bMoto uliwaangamiza vijana wao,
na wanawali wao hawakuimbiwa nyimbo za arusi,
64 cmakuhani wao waliuawa kwa upanga,
wala wajane wao hawakuweza kulia.

65 dNdipo Bwana alipoamka kama vile kuamka usingizini,
kama vile mtu aamkavyo kutoka kwenye bumbuazi la mvinyo.
66 eAliwapiga na kuwashinda adui zake,
akawatia katika aibu ya milele.
67 fNdipo alipozikataa hema za Yosefu,
hakulichagua kabila la Efraimu,
68 glakini alilichagua kabila la Yuda,
Mlima Sayuni, ambao aliupenda.
69 hAlijenga patakatifu pake kama vilele,
kama dunia ambayo aliimarisha milele.
70 iAkamchagua Daudi mtumishi wake
na kumtoa kwenye mazizi ya kondoo.
71 jKutoka kuchunga kondoo alimleta
kuwa mchungaji wa watu wake Yakobo,
wa Israeli urithi wake.
Copyright information for SwhNEN