Psalms 74:3-7
3 aGeuza hatua zako kuelekea magofu haya ya kudumu,uharibifu wote huu ambao adui ameuleta pale patakatifu.
4 bAdui zako wamenguruma pale ulipokutana nasi,
wanaweka bendera zao kama alama.
5 cWalifanya kama watu wanaotumia mashoka
kukata kichaka cha miti.
6 dWalivunjavunja milango yote iliyonakshiwa
kwa mashoka na vishoka vyao.
7 eWaliteketeza kabisa mahali pako patakatifu,
wakayanajisi makao ya Jina lako.
Copyright information for
SwhNEN