‏ Psalms 72:10-15

10 aWafalme wa Tarshishi na wa pwani za mbali
watamletea kodi;
wafalme wa Sheba na Seba
watampa zawadi.
11 bWafalme wote watamsujudia
na mataifa yote yatamtumikia.

12Kwa maana atamwokoa mhitaji anayemlilia,
aliyeonewa asiye na wa kumsaidia.
13 cAtawahurumia wanyonge na wahitaji
na kuwaokoa wahitaji kutoka mauti.
14 dAtawaokoa kutoka uonevu na ukatili,
kwani damu yao ni ya thamani machoni pake.

15 eAishi maisha marefu!
Na apewe dhahabu ya Sheba.
Watu wamwombee daima
na kumbariki mchana kutwa.
Copyright information for SwhNEN