Psalms 7:11-16
11 aMungu ni mwamuzi mwenye haki,Mungu aghadhibikaye kila siku.
12 bKama hakutuhurumia,
atanoa upanga wake,
ataupinda na kuufunga uzi upinde wake.
13 cAmeandaa silaha zake kali,
ameweka tayari mishale yake ya moto.
14 dYeye aliye na mimba ya uovu
na achukuaye mimba ya ghasia huzaa uongo.
15 eYeye achimbaye shimo na kulifukua
hutumbukia katika shimo alilochimba mwenyewe.
16 fGhasia azianzishazo humrudia mwenyewe,
ukatili wake humrudia kichwani.
Copyright information for
SwhNEN