‏ Psalms 7:11-14

11 aMungu ni mwamuzi mwenye haki,
Mungu aghadhibikaye kila siku.
12 bKama hakutuhurumia,
atanoa upanga wake,
ataupinda na kuufunga uzi upinde wake.
13 cAmeandaa silaha zake kali,
ameweka tayari mishale yake ya moto.

14 dYeye aliye na mimba ya uovu
na achukuaye mimba ya ghasia huzaa uongo.

Copyright information for SwhNEN
The selected Bible will not be clickable as it does not support the Vocabulary feature. The vocabulary is available by hovering over the verse number.