Psalms 65:9-13
9 aWaitunza nchi na kuinyeshea,
waitajirisha kwa wingi.
Vijito vya Mungu vimejaa maji
ili kuwapa watu nafaka,
kwa maana wewe umeviamuru.
10 bUmeilowesha mifereji yake
na kusawazisha kingo zake;
umeilainisha kwa manyunyu
na kuibariki mimea yake.
11 cUmeuvika mwaka taji ya baraka,
magari yako yanafurika kwa wingi.
12 dMbuga za majani za jangwani umezineemesha;
vilima vimevikwa furaha.
13 ePenye nyanda za malisho pamejaa makundi ya wanyama,
na mabonde yamepambwa kwa mavuno;
vyote vinashangilia kwa furaha na kuimba.
Copyright information for
SwhNEN