‏ Psalms 59:5-13

5 aEe Bwana Mwenye Nguvu Zote, Mungu wa Israeli!
Zinduka uyaadhibu mataifa yote,
usionyeshe huruma kwa wasaliti.

6 bHurudi wakati wa jioni,
wakibweka kama mbwa,
wakiuzurura mji.
7 cTazama yale wanayotema kutoka vinywa vyao,
hutema upanga kutoka midomo yao,
nao husema, “Ni nani atakayetusikia?”
8 dLakini wewe, Bwana, uwacheke;
unayadharau mataifa hayo yote.

9 eEe nguvu yangu, ninakutazama wewe,
wewe, Ee Mungu, ndiwe ngome yangu,
10Mungu wangu unipendaye.

Mungu atanitangulia,
naye atanifanya niwachekelee
wale wanaonisingizia.
11 fLakini usiwaue, Ee Bwana, ngao yetu,
au sivyo watu wangu watasahau.
Katika uwezo wako wafanye watangetange
na uwashushe chini.
12 gKwa ajili ya dhambi za vinywa vyao,
kwa ajili ya maneno ya midomo yao,
waache wanaswe katika kiburi chao.
Kwa ajili ya laana na uongo wanaotamka,
13 hwateketeze katika ghadhabu,
wateketeze hadi wasiwepo tena.
Ndipo itakapofahamika katika miisho ya dunia
kwamba Mungu anatawala juu ya Yakobo.
Copyright information for SwhNEN