Psalms 57:1-3
Kuomba Msaada
Kwa mwimbishaji. Mtindo wa “Usiharibu!” Utenzi wa Daudi. Baada ya kumponyoka Sauli pangoni.
1 aUnihurumie, Ee Mungu, unihurumie,kwa maana nafsi yangu inakukimbilia.
Chini ya uvuli wa mbawa zako nitakimbilia
mpaka maafa yapite.
2 bNamlilia Mungu Aliye Juu Sana,
Mungu atimizaye makusudi yake kwangu.
3 cHutumana kutoka mbinguni na kuniokoa,
akiwakemea wale wanaonifuatilia vikali;
Mungu huutuma upendo wake na uaminifu wake.
Copyright information for
SwhNEN