‏ Psalms 53:1-3

Uovu Wa Wanadamu

(Zaburi 14)

Kwa mwimbishaji. Mtindo wa mahalathi. Utenzi wa Daudi.

1 aMpumbavu anasema moyoni mwake,
“Hakuna Mungu.”
Wameharibika, na njia zao ni za uovu kabisa,
hakuna hata mmoja atendaye mema.

2 bMungu anawachungulia wanadamu chini
kutoka mbinguni
aone kama wako wenye akili,
wowote wanaomtafuta Mungu.
3 cKila mmoja amegeukia mbali,
wameharibika wote pamoja,
hakuna atendaye mema.
Naam, hakuna hata mmoja!
Copyright information for SwhNEN