‏ Psalms 52:5-7


5 aHakika Mungu atakushusha chini
kwa maangamizi ya milele:
atakunyakua na kukuondoa kwa nguvu
kutoka hema yako,
atakungʼoa kutoka nchi ya walio hai.
6 bWenye haki wataona na kuogopa,
watamcheka, wakisema,
7 c“Huyu ni yule mtu ambaye
hakumfanya Mungu kuwa ngome yake,
bali alitumainia wingi wa utajiri wake,
na akawa hodari kwa kuwaangamiza wengine!”
Copyright information for SwhNEN