Psalms 51:15-19
15 aEe Bwana, fungua midomo yangu,na kinywa changu kitatangaza sifa zako.
16 bWewe hupendezwi na dhabihu, au ningaliileta,
hufurahii sadaka za kuteketezwa.
17 cBali dhabihu za Mungu ni roho iliyovunjika,
moyo uliovunjika wenye toba,
Ee Mungu, hutaudharau.
18 dKwa wema wa radhi yako uifanye Sayuni istawi,
ukazijenge upya kuta za Yerusalemu.
19Hapo ndipo kutakapokuwa na dhabihu za haki,
sadaka nzima za kuteketezwa za kukupendeza sana,
pia mafahali watatolewa
madhabahuni mwako.
Copyright information for
SwhNEN