Psalms 48:1-3
Sayuni, Mji Wa Mungu
Wimbo. Zaburi ya wana wa Kora.
1 a Bwana ni mkuu, anayestahili kusifiwa sana,katika mji wa Mungu wetu,
mlima wake mtakatifu.
2 bNi mzuri katika kuinuka kwake juu sana,
furaha ya dunia yote.
Kama vilele vya juu sana vya Safoni ▼
▼Safoni inaweza ikawa na maana ya mlima mtakatifu au upande wa kaskazini.
ni Mlima Sayuni,mji wa Mfalme Mkuu.
3 dMungu yuko katika ngome zake;
amejionyesha mwenyewe kuwa ngome yake.
Copyright information for
SwhNEN