Psalms 46:7-11
7 a Bwana Mwenye Nguvu Zote yu pamoja nasi,
Mungu wa Yakobo ni ngome yetu.
8 bNjooni mkaone kazi za Bwana
jinsi alivyofanya ukiwa katika nchi.
9 cAnakomesha vita hata miisho ya dunia,
anakata upinde na kuvunjavunja mkuki,
anateketeza ngao kwa moto.
10 d“Tulieni, mjue ya kwamba mimi ndimi Mungu;
nitatukuzwa katikati ya mataifa,
nitatukuzwa katika dunia.”
11 Bwana Mwenye Nguvu Zote yu pamoja nasi;
Mungu wa Yakobo ni ngome yetu.
Copyright information for
SwhNEN