Psalms 46:2-6
2 aKwa hiyo hatutaogopa, hata kama dunia ikiondolewanayo milima ikiangukia moyoni mwa bahari.
3 bHata kama maji yake yatanguruma na kuumuka,
milima nayo ikitetemeka kwa mawimbi yake.
4 cKuna mto ambao vijito vyake vinaufurahisha mji wa Mungu,
mahali patakatifu ambako Aliye Juu Sana anaishi.
5 dMungu yuko katikati yake, hautaanguka,
Mungu atausaidia asubuhi na mapema.
6 eMataifa yanafanya ghasia, falme zinaanguka,
Yeye huinua sauti yake, dunia ikayeyuka.
Copyright information for
SwhNEN