Psalms 44:3-7
3 aSio kwa upanga wao waliipata nchi,wala si mkono wao uliwapatia ushindi;
ilikuwa ni kitanga cha mkono wako wa kuume,
na nuru ya uso wako,
kwa kuwa uliwapenda.
4 bWewe ni mfalme wangu na Mungu wangu,
unayeamuru ushindi kwa Yakobo.
5 cKwa uwezo wako tunawasukuma nyuma watesi wetu;
kwa jina lako tunawakanyaga adui zetu.
6 dSiutumaini upinde wangu,
upanga wangu hauniletei ushindi;
7 ebali wewe unatupa ushindi juu ya adui zetu,
unawaaibisha watesi wetu.
Copyright information for
SwhNEN