‏ Psalms 34:12-16

12 aYeyote kati yenu anayependa uzima
na kutamani kuziona siku nyingi njema,
13 bbasi auzuie ulimi wake na mabaya,
na midomo yake kutokana na kusema uongo.
14 cAache uovu, atende mema,
aitafute amani na kuifuatilia.

15 dMacho ya Bwana huwaelekea wenye haki,
na masikio yake yako makini kusikiliza kilio chao.
16 eUso wa Bwana uko kinyume na watendao maovu,
ili kufuta kumbukumbu lao duniani.
Copyright information for SwhNEN