‏ Psalms 33:6-9


6 aKwa neno la Bwana mbingu ziliumbwa,
jeshi lao la angani kwa pumzi ya kinywa chake.
7 bAmeyakusanya maji ya bahari
kama kwenye chungu;
vilindi vya bahari
ameviweka katika ghala.
8 cDunia yote na imwogope Bwana,
watu wote wa dunia wamche.
9 dKwa maana Mungu alisema, na ikawa,
aliamuru na ikasimama imara.
Copyright information for SwhNEN