Psalms 3:2-7
2 aWengi wanasema juu yangu,“Mungu hatamwokoa.”
3 bLakini wewe, Ee Bwana, ni ngao pande zote;
umeniwekea utukufu na kuinua kichwa changu.
4 cNinamlilia Bwana kwa sauti kuu,
naye ananijibu kutoka mlima wake mtakatifu.
5 dNinajilaza na kupata usingizi;
naamka tena, kwa maana Bwana hunitegemeza.
6 eSitaogopa makumi elfu ya adui,
wanaojipanga dhidi yangu kila upande.
7 fEe Bwana, amka!
Niokoe, Ee Mungu wangu!
Wapige adui zangu wote kwenye taya,
vunja meno ya waovu.
Copyright information for
SwhNEN