Psalms 18:37-42
37 aNiliwafuatia adui zangu na nikawapata,
sikurudi nyuma mpaka walipoangamizwa.
38 bNiliwaseta hata hawakuweza kuinuka tena;
walianguka chini ya miguu yangu.
39 cUlinivika nguvu kwa ajili ya kupigana vita;
uliwafanya adui zangu wasujudu miguuni pangu.
40 dUliwafanya adui zangu wageuke na kukimbia,
nami nikawaangamiza adui zangu.
41 eWalipiga yowe, lakini hapakuwepo na yeyote wa kuwaokoa;
walimlilia Bwana, lakini hakuwajibu.
42 fNiliwaponda kama mavumbi yanayopeperushwa na upepo;
niliwamwaga nje kama tope barabarani.
Copyright information for
SwhNEN