Psalms 16:8-11
8 a bNimemweka Bwana mbele yangu daima.Kwa sababu yuko mkono wangu wa kuume,
sitatikisika.
9 cKwa hiyo moyo wangu unafurahia, na ulimi wangu unashangilia;
mwili wangu nao utapumzika salama,
10 dkwa maana hutaniacha kaburini,
wala hutamwacha Mtakatifu Wako kuona uharibifu.
11 eUmenijulisha njia ya uzima;
utanijaza na furaha mbele zako,
pamoja na furaha za milele
katika mkono wako wa kuume.
Copyright information for
SwhNEN