Psalms 144:13-15
13 aGhala zetu zitajazwaaina zote za mahitaji.
Kondoo zetu watazaa kwa maelfu,
kwa makumi ya maelfu katika mashamba yetu;
14 bmaksai wetu watakokota
mizigo mizito.
Hakutakuwa na kubomoka kuta,
hakuna kuchukuliwa mateka,
wala kilio cha taabu
katika barabara zetu.
15 cHeri watu ambao hili ni kweli;
heri wale ambao Bwana ni Mungu wao.
Copyright information for
SwhNEN