‏ Psalms 132:1-5

Maskani Ya Mungu Ya Milele Katika Sayuni

Wimbo wa kwenda juu.

1Ee Bwana, mkumbuke Daudi
na taabu zote alizozistahimili.

2 aAliapa kiapo kwa Bwana
na akaweka nadhiri kwa Yule Mwenye Nguvu wa Yakobo:
3 b“Sitaingia nyumbani mwangu
au kwenda kitandani mwangu:
4 csitaruhusu usingizi katika macho yangu,
wala kope zangu kusinzia,
5 dmpaka nitakapompatia Bwana mahali,
makao kwa ajili ya Yule Mwenye Nguvu wa Yakobo.”
Copyright information for SwhNEN