Psalms 130:4-7
4 aLakini kwako kuna msamaha,kwa hiyo wewe unaogopwa.
5 bNamngojea Bwana, nafsi yangu inangojea,
katika neno lake naweka tumaini langu.
6 cNafsi yangu inamngojea Bwana
kuliko walinzi waingojeavyo asubuhi,
naam, kuliko walinzi
waingojeavyo asubuhi.
7 dEe Israeli, mtumaini Bwana,
maana kwa Bwana kuna upendo usiokoma,
na kwake kuna ukombozi kamili.
Copyright information for
SwhNEN