‏ Psalms 128:2-4

2 aUtakula matunda ya kazi yako;
baraka na mafanikio vitakuwa vyako.
3 bMke wako atakuwa kama mzabibu uzaao
ndani ya nyumba yako;
wana wako watakuwa kama machipukizi ya mizeituni
kuizunguka meza yako.
4 cHivyo ndivyo atakavyobarikiwa
mtu amchaye Bwana.
Copyright information for SwhNEN