Psalms 128:1-4
Thawabu Ya Kumtii Bwana
Wimbo wa kwenda juu.
1 aHeri ni wale wote wamchao Bwana,waendao katika njia zake.
2 bUtakula matunda ya kazi yako;
baraka na mafanikio vitakuwa vyako.
3 cMke wako atakuwa kama mzabibu uzaao
ndani ya nyumba yako;
wana wako watakuwa kama machipukizi ya mizeituni
kuizunguka meza yako.
4 dHivyo ndivyo atakavyobarikiwa
mtu amchaye Bwana.
Copyright information for
SwhNEN