‏ Psalms 107:10-14


10 aWengine walikaa gizani na katika huzuni kuu,
wafungwa wakiteseka katika minyororo,
11 bkwa sababu walikuwa wameasi
dhidi ya maneno ya Mungu
na kudharau shauri
la Aliye Juu Sana.
12 cAliwatumikisha kwa kazi ngumu;
walijikwaa na hapakuwepo yeyote wa kuwasaidia.
13 dNdipo walipomlilia Bwana katika shida yao,
naye akawaokoa kutoka taabu yao.
14 eAkawatoa katika giza na huzuni kuu
na akavunja minyororo yao.
Copyright information for SwhNEN