Psalms 105:42-45
42 aKwa maana alikumbuka ahadi yake takatifu,
aliyompa Abrahamu mtumishi wake.
43 bAliwatoa watu wake kwa furaha,
wateule wake kwa kelele za shangwe,
44 cakawapa nchi za mataifa, wakawa warithi
wa mali wengine walikuwa wameitaabikia:
45 dalifanya haya ili wayashike mausia yake
na kuzitii sheria zake.
Msifuni Bwana. ▼
▼Msifuni Bwana kwa Kiebrania ni Hallelu Yah.
Copyright information for
SwhNEN