Psalms 104:5-13
5 aAmeiweka dunia kwenye misingi yake,
haiwezi kamwe kuondoshwa.
6 bUliifunika kwa kilindi kama kwa vazi,
maji yalisimama juu ya milima.
7 cLakini kwa kukemea kwako maji yalikimbia,
kwa sauti ya radi yako yakatoroka,
8 dyakapanda milima, yakateremka mabondeni,
hadi mahali pale ulipoyakusudia.
9 eUliyawekea mpaka ambao hayawezi kuuvuka,
kamwe hayataifunika dunia tena.
10 fHuzifanya chemchemi zimwage maji mabondeni,
hutiririka kati ya milima.
11 gHuwapa maji wanyama wote wa kondeni,
punda-mwitu huzima kiu yao.
12 hNdege wa angani hufanya viota kando ya maji,
huimba katikati ya matawi.
13 iHuinyeshea milima kutoka orofa zake,
dunia inatoshelezwa kwa matunda ya kazi yake.
Copyright information for
SwhNEN