‏ Psalms 103:1-13

Upendo Wa Mungu

Zaburi ya Daudi.

1 aEe nafsi yangu, umhimidi Bwana.
Vyote vilivyomo ndani yangu
vilihimidi jina lake takatifu.
2 bEe nafsi yangu, umhimidi Bwana,
wala usisahau wema wake wote,
3 cakusamehe dhambi zako zote,
akuponya magonjwa yako yote,
4 daukomboa uhai wako na kaburi,
akuvika taji ya upendo na huruma,
5 eatosheleza mahitaji yako kwa vitu vyema,
ili ujana wako uhuishwe kama wa tai.

6 f Bwana hutenda haki,
naye huwapa hukumu ya haki wote wanaoonewa.

7 gAlijulisha Mose njia zake,
na wana wa Israeli matendo yake.
8 h Bwana ni mwingi wa huruma na mwenye neema;
si mwepesi wa hasira, bali amejaa upendo.
9 iYeye hatalaumu siku zote,
wala haweki hasira yake milele,
10 jyeye hatutendei kulingana na dhambi zetu
wala hatupatilizi kwa kadiri ya maovu yetu.
11 kKama vile mbingu zilivyo juu ya dunia sana,
ndivyo wema wake ulivyo mwingi kwa wanaomcha;
12 lkama mashariki ilivyo mbali na magharibi,
ndivyo Mungu alivyoziweka dhambi zetu mbali nasi.
13 mKama baba alivyo na huruma kwa watoto wake,
ndivyo Bwana anavyowahurumia wale wanaomcha;
Copyright information for SwhNEN