‏ Psalms 102:22-27

22 awakati mataifa na falme zitakapokusanyika
ili kumwabudu Bwana.

23 bKatika kuishi kwangu alivunja nguvu zangu,
akafupisha siku zangu.
24 cNdipo niliposema:
“Ee Mungu wangu, usinichukue katikati ya siku zangu;
miaka yako inaendelea vizazi vyote.
25 dHapo mwanzo uliweka misingi ya dunia,
nazo mbingu ni kazi ya mikono yako.
26 eHizi zitatoweka, lakini wewe utadumu,
zote zitachakaa kama vazi.
Utazibadilisha kama nguo
nazo zitaondoshwa.
27 fLakini wewe, U yeye yule,
nayo miaka yako haikomi kamwe.
Copyright information for SwhNEN