Proverbs 8:10-19
10 aChagua mafundisho yangu badala ya fedha,maarifa badala ya dhahabu safi,
11 bkwa maana hekima ina thamani kuliko marijani
na hakuna chochote unachohitaji kinacholingana naye.
12 c“Mimi hekima, nakaa pamoja na busara;
ninamiliki maarifa na busara.
13 dKumcha Bwana ni kuchukia uovu;
ninachukia kiburi na majivuno,
tabia mbaya na mazungumzo potovu.
14 eUshauri na hukumu sahihi ni vyangu;
nina ufahamu na nina nguvu.
15 fKwa msaada wangu wafalme hutawala
na watawala hutunga sheria zilizo za haki,
16 gkwa msaada wangu wakuu hutawala,
na wenye vyeo wote watawalao dunia.
17 hNawapenda wale wanipendao,
na wale wanitafutao kwa bidii wataniona.
18 iUtajiri na heshima viko kwangu,
utajiri udumuo na mafanikio.
19 jTunda langu ni bora kuliko dhahabu safi;
kile nitoacho hupita fedha iliyo bora.
Copyright information for
SwhNEN