Proverbs 29:2-12
2 aWenye haki wanapostawi, watu hufurahi;
waovu watawalapo, watu hulia kwa huzuni.
3 bMtu apendaye hekima huleta furaha kwa baba yake,
bali aambatanaye na makahaba hutapanya mali yake.
4 cKwa haki mfalme huipa nchi uthabiti,
bali mfalme aliye na tamaa ya rushwa huiangamiza.
5 dYeyote amsifuye jirani yake isivyostahili,
anautandaza wavu kuitega miguu yake.
6 eMtu mbaya hutegwa na dhambi yake mwenyewe
bali mwenye haki huweza kuimba na kufurahi.
7 fMwenye haki hujali haki kwa ajili ya maskini,
bali mwovu hajishughulishi na hilo.
8 gWenye mzaha huuchochea mji,
bali watu wenye hekima hugeuzia mbali hasira.
9 hKama mwenye hekima akienda mahakamani na mpumbavu,
mpumbavu hukasirika na kudhihaki, wala hakuna amani.
10 iWatu wamwagao damu humchukia mtu mwadilifu
na hutafuta kumuua mtu mnyofu.
11 jMpumbavu huonyesha hasira yake yote,
bali mwenye hekima hujizuia.
12 kKama mtawala akisikiliza uongo,
maafisa wake wote huwa waovu.
Copyright information for
SwhNEN