Proverbs 2:6-10
6 aKwa maana Bwana hutoa hekima,na kinywani mwake hutoka maarifa na ufahamu.
7 bAnahifadhi ushindi kwa ajili ya mwadilifu,
yeye ni ngao kwa wale wasio na lawama,
8 ckwa kuwa hulinda mwenendo wa mwenye haki
na kuhifadhi njia ya waaminifu wake.
9 dNdipo utafahamu lipi lililo kweli na haki
na sawa: yaani kila njia nzuri.
10 eKwa maana hekima itaingia moyoni mwako,
nayo maarifa yataifurahisha nafsi yako.
Copyright information for
SwhNEN