Proverbs 19:5-10
5 aShahidi wa uongo hataacha kuadhibiwa,
naye amwagaye uongo hataachwa huru.
6 bWengi hujipendekeza kwa mtawala
na kila mmoja ni rafiki wa mtu atoaye zawadi.
7 cMtu maskini huepukwa na ndugu zake wote:
Je, marafiki zake watamkwepa kiasi gani!
Ingawa huwafuata kwa kuwasihi,
hawapatikani popote.
8 dYeye apataye hekima huipenda nafsi yake mwenyewe,
yeye ahifadhiye ufahamu hustawi.
9 eShahidi wa uongo hataacha kuadhibiwa,
naye amwagaye uongo ataangamia.
10 fHaistahili mpumbavu kuishi katika anasa,
itakuwa vibaya kiasi gani
kwa mtumwa kuwatawala wakuu.
Copyright information for
SwhNEN