‏ Proverbs 1:10-19


10 aMwanangu, kama wenye dhambi wakikushawishi,
usikubaliane nao.
11 bKama wakisema, “Twende tufuatane;
tukamvizie mtu na kumwaga damu,
njoo tukavizie nafsi isiyo na hatia;
12 ctuwameze wakiwa hai kama kaburi,
Kaburi hapa maana yake ni Kuzimu, kwa Kiebrania ni Sheol.

wakiwa wazima kama wale wanaotumbukia shimoni.
13Tutapata aina zote za vitu vya thamani
na kujaza nyumba zetu kwa nyara.
14 eNjoo ushirikiane nasi,
vitu vyote tutakavyopata tutagawana.”
15 fMwanangu, usiandamane nao.
Usiweke mguu wako katika njia zao,
16 gkwa kuwa miguu yao hukimbilia kwenye dhambi,
ni wepesi kumwaga damu.
17Tazama ni jinsi gani ilivyo kazi bure kutandaza wavu
wakati ndege wote wanakuona!
18 hWatu hawa huvizia kumwaga damu yao wenyewe;
hujivizia tu wenyewe!
19 iHuu ndio mwisho wa wote ambao wanajipatia mali kwa hila;
huuondoa uhai wa wale wenye mali.

Copyright information for SwhNEN
The selected Bible will not be clickable as it does not support the Vocabulary feature. The vocabulary is available by hovering over the verse number.

Everyone uses cookies. We do too! Cookies are little bits of information stored on your computer which help us give you a better experience. You can find out more by reading the STEPBible cookie policy.