‏ Obadiah 11-12

11 aSiku ile ulisimama mbali ukiangalia
wakati wageni walipojichukulia utajiri wake
na watu wa nchi nyingine walipoingia malango yake
wakipiga kura kwa ajili ya Yerusalemu,
ulikuwa kama mmoja wao.
12 bUsingemdharau ndugu yako
katika siku ya msiba wake,
wala kufurahia juu ya watu wa Yuda
katika siku ya maangamizi yao,
wala kujigamba sana
katika siku ya taabu yao.
Copyright information for SwhNEN