Numbers 6:23-27
23 a“Mwambie Aroni na wanawe, ‘Hivi ndivyo mtakavyowabariki Waisraeli. Waambieni:24 b“ ‘ “Bwana akubariki
na kukulinda;
25 c Bwana akuangazie nuru ya uso wake
na kukufadhili;
26 d Bwana akugeuzie uso wake
na kukupa amani.” ’
27 e“Hivyo wataliweka Jina langu juu ya Waisraeli, nami nitawabariki.”
Copyright information for
SwhNEN