Numbers 33:3-49
3 aWaisraeli walisafiri kutoka Ramesesi katika siku ya kumi na tano ya mwezi wa kwanza, siku iliyofuata Pasaka. Walitembea kwa ujasiri wazi mbele ya Wamisri wote, 4 bwaliokuwa wakizika wazaliwa wao wa kwanza wote, ambao Bwana alikuwa amewaua katikati yao, kwa kuwa Bwana alikuwa ameleta hukumu juu ya miungu yao.5 cWaisraeli waliondoka Ramesesi na kupiga kambi huko Sukothi.
6 dWakaondoka Sukothi na kupiga kambi huko Ethamu, pembeni mwa jangwa.
7 eWakaondoka Ethamu, wakageuka wakarudi Pi-Hahirothi, hadi mashariki ya Baal-Sefoni, wakapiga kambi yao karibu na Migdoli.
8 fWakaondoka Pi-Hahirothi wakapita katikati ya bahari mpaka jangwani, na baada ya kusafiri kwa siku tatu katika Jangwa la Ethamu, walipiga kambi huko Mara.
9 gWakaondoka Mara wakaenda Elimu, mahali ambapo palikuwa na chemchemi kumi na mbili na mitende sabini, huko wakapiga kambi.
10 hWakaondoka Elimu na kupiga kambi kando ya Bahari ya Shamu.
11 iWakaondoka kando ya Bahari ya Shamu na kupiga kambi katika Jangwa la Sini.
12Wakaondoka katika Jangwa la Sini, wakapiga kambi huko Dofka.
13Wakaondoka Dofka, wakapiga kambi huko Alushi.
14 jWakaondoka Alushi, wakapiga kambi Refidimu, mahali ambapo hapakuwa na maji kwa ajili ya watu kunywa.
15 kWakaondoka Refidimu na kupiga kambi katika Jangwa la Sinai.
16 lWakaondoka katika Jangwa la Sinai na kupiga kambi huko Kibroth-Hataava.
17 mWakaondoka Kibroth-Hataava na kupiga kambi huko Haserothi.
18 nWakaondoka Haserothi na kupiga kambi huko Rithma.
19Wakaondoka Rithma na kupiga kambi huko Rimon-Peresi.
20 oWakaondoka Rimon-Peresi na kupiga kambi huko Libna.
21Wakaondoka Libna na kupiga kambi huko Risa.
22Wakaondoka Risa na kupiga kambi huko Kehelatha.
23Wakaondoka Kehelatha na kupiga kambi kwenye mlima Sheferi.
24Wakaondoka kwenye mlima Sheferi na kupiga kambi huko Harada.
25Wakaondoka Harada na kupiga kambi huko Makelothi.
26Wakaondoka Makelothi na kupiga kambi huko Tahathi.
27Wakaondoka Tahathi na kupiga kambi huko Tera.
28Wakaondoka Tera na kupiga kambi huko Mithka.
29Wakaondoka Mithka na kupiga kambi huko Hashmona.
30 pWakaondoka Hashmona na kupiga kambi Moserothi.
31 qWakaondoka Moserothi na kupiga kambi huko Bene-Yakani.
32 rWakaondoka Bene-Yakani na kupiga kambi huko Hor-Hagidgadi.
33 sWakaondoka Hor-Hagidgadi na kupiga kambi huko Yotbatha.
34Wakaondoka Yotbatha na kupiga kambi huko Abrona.
35 tWakaondoka Abrona na kupiga kambi huko Esion-Geberi.
36 uWakaondoka Esion-Geberi na kupiga kambi huko Kadeshi katika Jangwa la Sini.
37 vWakaondoka Kadeshi na kupiga kambi kwenye Mlima Hori, mpakani mwa Edomu. 38 wKwa amri ya Bwana, kuhani Aroni alipanda Mlima Hori, mahali alipofia katika siku ya kwanza ya mwezi wa tano, mwaka wa arobaini baada ya Waisraeli kutoka Misri. 39Aroni alikufa juu ya Mlima Hori akiwa na umri wa miaka 123.
40 xMfalme Mkanaani wa Aradi, ambaye aliishi huko Negebu ya Kanaani, akasikia kwamba Waisraeli wanakuja.
41Wakaondoka kwenye mlima Hori na kupiga kambi huko Salmona.
42Wakaondoka Salmona, wakapiga kambi huko Punoni.
43 yWakaondoka Punoni, wakapiga kambi huko Obothi.
44 zWakaondoka Obothi, wakapiga kambi huko Iye-Abarimu, mipakani mwa Moabu.
45 aaWakaondoka Iye-Abarimu, wakapiga kambi huko Dibon-Gadi.
46 abWakaondoka Dibon-Gadi na kupiga kambi huko Almon-Diblathaimu.
47 acWakaondoka Almon-Diblathaimu na kupiga kambi katika milima ya Abarimu, karibu na Nebo.
48 adWakaondoka kwenye milima ya Abarimu na kupiga kambi kwenye tambarare ya Moabu, kando ya Yordani ngʼambo ya Yeriko. 49 aeHuko kwenye tambarare za Moabu walipiga kambi kandokando ya Mto Yordani, kuanzia Beth-Yeshimothi mpaka Abel-Shitimu.
Copyright information for
SwhNEN