‏ Numbers 3:5-37

5 Bwana akamwambia Mose, 6 a“Walete watu wa kabila la Lawi mbele ya Aroni kuhani ili wamsaidie. 7 bWatafanya huduma kwa ajili yake na kwa jumuiya yote katika Hema la Kukutania kwa kufanya kazi za Maskani. 8Watatunza samani zote za Hema la Kukutania, wakitimiza wajibu wa kuhudumia Waisraeli kwa kufanya kazi ya Maskani. 9 cWakabidhi Walawi kwa Aroni na wanawe; hao ndio Waisraeli ambao wanakabidhiwa kwake kabisa. 10 dWaweke Aroni na wanawe kuhudumu kama makuhani; mtu mwingine yeyote atakayesogea mahali patakatifu ni lazima auawe.”

11 Bwana akamwambia Mose, 12 e“Nimewatwaa Walawi kutoka miongoni mwa Waisraeli badala ya mzaliwa wa kwanza wa kiume wa kila mwanamke wa Mwisraeli. Walawi ni wangu, 13 fkwa kuwa wazaliwa wote wa kwanza ni wangu. Nilipowaua wazaliwa wa kwanza huko Misri, nilimtenga kila mzaliwa wa kwanza katika Israeli awe wangu, akiwa mwanadamu au mnyama. Watakuwa wangu. Mimi ndimi Bwana.”

14 Bwana akamwambia Mose katika Jangwa la Sinai, 15 g“Wahesabu Walawi kwa jamaa zao na koo zao. Mhesabu kila mwanaume mwenye umri wa mwezi mmoja au zaidi.” 16Kwa hiyo Mose akawahesabu, kama alivyoamriwa na neno la Bwana.

17 hHaya yalikuwa majina ya wana wa Lawi:
Gershoni, Kohathi na Merari.
18 iHaya ndiyo yaliyokuwa majina ya koo za Wagershoni:
Libni na Shimei.
19 jKoo za Wakohathi zilikuwa ni:
Amramu, Ishari, Hebroni na Uzieli.
20 kKoo za Wamerari zilikuwa ni:
Mahli na Mushi.
Hizi ndizo zilizokuwa koo za Walawi, kufuatana na jamaa zao.

21 lKulikuwa na koo za Walibni na Washimei kwa Gershoni; hizi ndizo zilizokuwa koo za Wagershoni. 22Idadi ya waume wote waliokuwa na mwezi mmoja au zaidi waliohesabiwa walikuwa 7,500. 23 mUkoo wa Wagershoni walitakiwa kuweka kambi zao upande wa magharibi, nyuma ya Maskani. 24Kiongozi wa jamaa za Wagershoni alikuwa Eliasafu mwana wa Laeli. 25 nKatika Hema la Kukutania, Wagershoni walikuwa na wajibu wa kutunza Maskani na hema, vifuniko vyake, pazia katika mlango wa kuingilia ndani ya Hema la Kukutania, 26 omapazia ya ua, pazia katika ingilio la ua unaozunguka Maskani na madhabahu, pamoja na kamba, na kila kinachohusika kwa matumizi yake.

27 pKwa Kohathi kulikuwepo koo za Waamramu, Waishari, Wahebroni na Wauzieli; hizi ndizo zilizokuwa koo za Wakohathi. 28 qHesabu ya waume wote wenye mwezi mmoja au zaidi ilikuwa watu 8,600. Wakohathi waliwajibika kutunza mahali patakatifu. 29 rKoo za Wakohathi zilitakiwa kuweka kambi zao upande wa kusini wa Maskani. 30 sKiongozi wa jamaa za koo za Wakohathi alikuwa Elisafani mwana wa Uzieli. 31 tWaliwajibika kutunza Sanduku la Agano, meza, kinara cha taa, madhabahu, na vile vyombo vya mahali patakatifu vinavyotumika kuhudumu, pazia, na kila kitu kinachohusika na matumizi yake. 32 uKiongozi mkuu wa Walawi alikuwa Eleazari mwana wa kuhani, Aroni. Aliwekwa juu ya wale waliowajibika kutunza mahali patakatifu.

33 vKwa Merari kulikuwa na koo za Wamahli na Wamushi; hizi zilikuwa koo za Merari. 34Hesabu ya waume wote wenye umri wa mwaka mmoja au zaidi waliohesabiwa walikuwa 6,200. 35 wKiongozi wa jamaa za koo za Wamerari alikuwa Surieli mwana wa Abihaili; hawa walitakiwa kuweka kambi zao upande wa kaskazini mwa Maskani. 36 xWamerari waliwekwa kutunza miimo ya Maskani, mataruma yake, nguzo, vitako na vifaa vyake vyote na kila kitu kilichohusika na matumizi yake, 37 yna pia nguzo za ua unaozunguka pamoja na vitako vyake, vigingi vya hema na kamba zake.

Copyright information for SwhNEN